Monday, 14 June 2021

WAZIRI PROF.MKUMBO ARIDHISHWA NA UWEKEZAJI ULIOFANYWA NA KAMPUNI YA BAKHRESA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI MAKURUNGE WILAYANI BAGAMOYO MKOANI PWANI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa (kushoto) pamoja Mkurugenzi wa mawasiliano wa makampuni ya Bakhresa ndugu Hussein Sufian (kulia).


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akipata maelezo ya namna umwagiliaji mashamba ya miwa unavyofanyika.


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) mara baada ya kuanza kikao na uongozi wa kiwanda cha sukari cha Bagamoyo.


Muonekano wa kiwanda kipya cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo ambacho kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi juni mwaka 2022 kwa kuzalisha tani elfu 30 hadi 35 kwa kuanzia.


Muonekano wa mashamba ya miwa katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo.

.............................................

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Bagamoyo ambacho uzalishaji wake unatarajiwa kuanza mwezi juni mwaka 2022 kwa kuzalisha tani elfu 30 hadi 35 kwa kuanzia na kitakapokamilika kitazalisha tani laki moja (100,000) kwa mwaka katika kukidhi mahitaji ya sukari nchini.

Mhe. Prof. Mkumbo ameyazungumza hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha sukari kilichopo Bagamoyo na kujionea mashamba ya miwa na mabwawa ya maji kwa ajili ya umwagiliaji wa miwa.

Mhe. Prof. Mkumbo amesema kuwa moja ya vipaumbele vya Serikali ni kuwekeza katika viwanda ambayo vitazalisha bidhaa ambazo tunazihitaji kwa kiasi kikubwa na moja ya bidhaa hizo ni sukari, kwa sasa tuna mahitaji ya sukari ambayo ni tani 655,000 kwa mwaka ambapo uzalishaji wa sasa kwa viwanda vyote vya sukari ni tani 386,000 mpaka mwezi Mei mwaka huu uzalishaji ulikuwa ni tani 256,000 ambayo ni asilimia 60 ya mahitaji yote ambapo asilimia 40 inabidi tuagize kutoka nje ya nchi.

Aidha Mhe. Prof. Mkumbo amesema kuwa kwa sasa Tanzania tuna viwanda vya sukari takribani vitano ambavyo vilikuwa vya serikali wakapewa sekta binafsi ili kuviendeleza, kiwanda hiki cha kuzalisha Sukari cha Bagamoyo ni cha umiliki wa sekta binafsi kwa asilimia 100.

Naye Mkurugenzi wa mawasiliano wa makampuni ya Bakhresa ambaye ndiye mratibu wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari Bagamoyo ndugu Hussein Sufian amesema mradi huo unahusisha maeneo makubwa mawili kuendeleza shamba la kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa kiwanda umefikia asilimia 90 na changamoto iliyopo ni ubovu wa miundombinu ya barabara kutoka makurunge hadi kiwandani na pia upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambapo wanashirikiana vyema na Wizara ya maji ambao wana mpango wa kujenga bwawa kwa ajili ya utatuzi wa changamoto hiyo. Aidha ameishukuru TANESCO ambapo kwa sasa umeme umekwishaunganishwa na hawatumii tena majenereta.

Ndugu Sufian ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kushughulikia changamoto wanazopata kwa wakati na kuipongeza serikali ya wilaya ya Bagamoyo kwa juhudi wanazofanya katika kuhakikisha kiwanda kinakamilika mapema kwa muda uliopangwa na kuanza kazi kwani kiwanda kwa awamu ya kwanza kinategemea kuajili wafanyakazi zaidi ya elfu moja (1,000) na baada ya awamu zote tatu kukamilika kiwanda kitaajili wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4,000).

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa amesema kuwa ofisi yake inashughulukia changamoto ya uvamizi wa ardhi kwa eneo walilopewa, na serikali ipo katika mpango wa kumuongezea eneo mwekezaji huyo mzawa kati ya hekta 12,000 zilizobakia baada ya kupewa hekta 10,000 ili kumaliza changamoto hiyo ya wavamizi wa ardhi.

...MWISHO...


Friday, 28 May 2021

UEFA FINAL GAME IN ENGLAND PITCH... CHELSEA vs MAN CITY

Ni masaa machache kushuhudia na kuikata kiu ya wanasoka wote Duniani kwa ujumla waliokaa kwa muda na wakingoja kujua ni nani atakuwa bigwa wa kumbe la Club Bingwa Barani Ulaya UEFA kati ya mahasimu wawili wa Ligi kuu Egland hapa inazungumziwa Chelsea na Manchester City

Thursday, 27 May 2021

Manchester United loss Europa agaist villarreal after 11 Penalt....

Moja kati ya tumaini kubwa lililokuwa likiwapa mashabiki wa Manchester United Duniani kote kiburi na jeuri ilikuwa kulichukua kombe maarufu duniani EUROPA LEAGUE.

Ila kama ilivyo ada kwamba siku huwa azigandi na ile misemo miwili maarufu kwenye mpira wa miguu zijulikanazo kama Mpira ni dakika Tisini Kweli zilianza kuanzia sekunde ya kwanza mpaka Dakika ya tisini ikiwa bado Mashabiki wa Manchester United wakiamini kwa timu waliyonayo basi bado wananafasi kubwa ya kupata ubingwa huo, ila kauli yapili ndiyo iliyowamaliza Manchester United (Mpira unadunda), Mambo yalikuwa magumu kwa timu zote mbili kupelekea dakika za nyongeza pia matokeo kuwa ni 1:1.

Haikuwa bahati kwa Manchester United kuingia kwenye Mikwaju ya penalt na hii ni baada ya Manchester kupoteza Mchezo huo na kulipoteza komba ambalo mashabiki wake duniani walikuwa wakilingoja, Nibaada ya Penalt 10 kuwa sawa kwenye Penalt ya 11 Villarreal wakaibuka washindi mara baada ya Golikipa wa Manchester United kukosa Penalt na Mwenzie wa Villarreal kushinda hivyo kupelekea Manchester kuwa nyuma ya Villarreal na kuwapa ruksa ya kutangazwa kuwa Mabingwa wapya wa kombe la Europa League

Thursday, 20 May 2021

DESKTOP SPECIFICATION FOR HOME AND OFFICE USE....

Hellow how are you there!, I hope you go through this post healthfully, Todays the world activity is converted to Computer based time to time, most of the work are done through the use of the computer thus the Computer become the Most Important device from personal level, office level, National level and Worldwide Level.

On this Post out Blogger try to explain Some if not all-Important factor to consider when buying a Desktop Computer for Home/Personal Use to office level.

MOTHERBOARD: Gigabyte B560M-DS3H Motherboard
POWER SUPPLY: Scaled appropriately to support delivered system with reasonable growth potential (In Win CE685 PC case with 300-watt 80PLUS certified power supply
CASE: In Win CE685 PC case with 300-watt 80PLUS certified power supply
CPU: Intel Core i5-11400 Processor
RAM: 8GB DDR4 2666 (PC4 21333) RAM (1 8GB DIMM) it is recommended the computer to have more than one RAM Slot.
NIC: On-board 10/100/1000 Mbps based Ethernet NIC
HDD: 250 GB Western Digital M.2 NVMe SSD Part # WDS250G2B0C
VIDEO: Integrated Intel HD Graphics with DVI Digital Output Interface
OPTICAL DRIVE: (optional)
AUDIO: Onboard HD audio (this is optional as not come with internal speaker but make sure the external speaker is working properly)
EXTERNALLY POWERED SATELLITE SPEAKERS: (optional)
6 EXTERNAL POWERED USB PORTS AND 2 ON FRONT OF CASE
OPERATING SYSTEM: Microsoft Windows 7 Home Basic (or other least expensive Microsoft Windows operating system) it can be above this OS not Limited to Maximum version only for Min-Version.
ALL APPROPRIATE CABLES NECESSARY HIDS: USB Optical mouse, mouse pad, USB keyboard, all necessary cables
WARRANTY 3-year parts and labor warranty on all components, and make sure the Condition for warranty is well explained on the manual book with your Device
MONITOR: 20″ Wide Screen LCD Monitor (1920×1080 native resolution) with DVI Digital Input Interface.

On the next Post we will describe the Factor for Personal Computer 🖥 (Laptop) For any Question, please Comment here down and our expert will come to chat with you direct to your email, also your allowed to ask for Specific Requirement of your Computer depend on what you want to do with it.

SIMBA FC DO or DIE SEASON 2

KAGERE; CHAMA; MIQUISO; BOKO; MORRISON TUMAINI LA SIMBA

Ikiwa ni siku mbili tuh simebaki kwa Simba kuipata hatima ya Timu yao kuendelea na michuano ya mabigwa afrika au kurudi kucheza mechi za ndani kama watani wao Yanga. Japo ni ngumu ila wachezaji wa Simba pamoja na Kocha wao Gomez wamesema haya katika mahojiono na waandishi tofauti tofauti wa habari "Nikweli tuna mlima mkubwa wa kupanda ili kuendelea na safari yetu ya michuano hii ya mabigwa wa soka barani Afrika lakini hatujalala wala kukata tamaa tangu tumerejea kutoka Afrika ya Kusini na tupo kwenye mazoezi ya kufa na kupona kuhakikisha tunapanda kilima hicho cha ushindi wa goli 5 kwa o katika uwanja wetu wa nyumbani Pale kwa Mkapa! na kurudisha imani ya mashabiki wetu ikiwa ni sambamba na kupata tiketi ya kuendelea katika hatua ya nusu fainali"

Hiyo ndio kauli ya Simba kwa ujumla kwa sasa ikiwa ni njia ya kutiana moyo na kuongeza maandalizi katika kuwania nafasi ya kuingia katika hatua ya nusu fainali na hatimaye fainali ya Kombe la mabingwa afrika.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Simba FC