Moja kati ya tumaini kubwa lililokuwa likiwapa mashabiki wa Manchester United Duniani kote kiburi na jeuri ilikuwa kulichukua kombe maarufu duniani EUROPA LEAGUE.
Ila kama ilivyo ada kwamba siku huwa azigandi na ile misemo miwili maarufu kwenye mpira wa miguu zijulikanazo kama Mpira ni dakika Tisini Kweli zilianza kuanzia sekunde ya kwanza mpaka Dakika ya tisini ikiwa bado Mashabiki wa Manchester United wakiamini kwa timu waliyonayo basi bado wananafasi kubwa ya kupata ubingwa huo, ila kauli yapili ndiyo iliyowamaliza Manchester United (Mpira unadunda), Mambo yalikuwa magumu kwa timu zote mbili kupelekea dakika za nyongeza pia matokeo kuwa ni 1:1.
Haikuwa bahati kwa Manchester United kuingia kwenye Mikwaju ya penalt na hii ni baada ya Manchester kupoteza Mchezo huo na kulipoteza komba ambalo mashabiki wake duniani walikuwa wakilingoja, Nibaada ya Penalt 10 kuwa sawa kwenye Penalt ya 11 Villarreal wakaibuka washindi mara baada ya Golikipa wa Manchester United kukosa Penalt na Mwenzie wa Villarreal kushinda hivyo kupelekea Manchester kuwa nyuma ya Villarreal na kuwapa ruksa ya kutangazwa kuwa Mabingwa wapya wa kombe la Europa League
No comments:
Post a Comment