Monday, 14 June 2021

WAZIRI PROF.MKUMBO ARIDHISHWA NA UWEKEZAJI ULIOFANYWA NA KAMPUNI YA BAKHRESA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI MAKURUNGE WILAYANI BAGAMOYO MKOANI PWANI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa (kushoto) pamoja Mkurugenzi wa mawasiliano wa makampuni ya Bakhresa ndugu Hussein Sufian (kulia).


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akipata maelezo ya namna umwagiliaji mashamba ya miwa unavyofanyika.


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) mara baada ya kuanza kikao na uongozi wa kiwanda cha sukari cha Bagamoyo.


Muonekano wa kiwanda kipya cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo ambacho kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi juni mwaka 2022 kwa kuzalisha tani elfu 30 hadi 35 kwa kuanzia.


Muonekano wa mashamba ya miwa katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo.

.............................................

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Bagamoyo ambacho uzalishaji wake unatarajiwa kuanza mwezi juni mwaka 2022 kwa kuzalisha tani elfu 30 hadi 35 kwa kuanzia na kitakapokamilika kitazalisha tani laki moja (100,000) kwa mwaka katika kukidhi mahitaji ya sukari nchini.

Mhe. Prof. Mkumbo ameyazungumza hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha sukari kilichopo Bagamoyo na kujionea mashamba ya miwa na mabwawa ya maji kwa ajili ya umwagiliaji wa miwa.

Mhe. Prof. Mkumbo amesema kuwa moja ya vipaumbele vya Serikali ni kuwekeza katika viwanda ambayo vitazalisha bidhaa ambazo tunazihitaji kwa kiasi kikubwa na moja ya bidhaa hizo ni sukari, kwa sasa tuna mahitaji ya sukari ambayo ni tani 655,000 kwa mwaka ambapo uzalishaji wa sasa kwa viwanda vyote vya sukari ni tani 386,000 mpaka mwezi Mei mwaka huu uzalishaji ulikuwa ni tani 256,000 ambayo ni asilimia 60 ya mahitaji yote ambapo asilimia 40 inabidi tuagize kutoka nje ya nchi.

Aidha Mhe. Prof. Mkumbo amesema kuwa kwa sasa Tanzania tuna viwanda vya sukari takribani vitano ambavyo vilikuwa vya serikali wakapewa sekta binafsi ili kuviendeleza, kiwanda hiki cha kuzalisha Sukari cha Bagamoyo ni cha umiliki wa sekta binafsi kwa asilimia 100.

Naye Mkurugenzi wa mawasiliano wa makampuni ya Bakhresa ambaye ndiye mratibu wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari Bagamoyo ndugu Hussein Sufian amesema mradi huo unahusisha maeneo makubwa mawili kuendeleza shamba la kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa kiwanda umefikia asilimia 90 na changamoto iliyopo ni ubovu wa miundombinu ya barabara kutoka makurunge hadi kiwandani na pia upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambapo wanashirikiana vyema na Wizara ya maji ambao wana mpango wa kujenga bwawa kwa ajili ya utatuzi wa changamoto hiyo. Aidha ameishukuru TANESCO ambapo kwa sasa umeme umekwishaunganishwa na hawatumii tena majenereta.

Ndugu Sufian ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kushughulikia changamoto wanazopata kwa wakati na kuipongeza serikali ya wilaya ya Bagamoyo kwa juhudi wanazofanya katika kuhakikisha kiwanda kinakamilika mapema kwa muda uliopangwa na kuanza kazi kwani kiwanda kwa awamu ya kwanza kinategemea kuajili wafanyakazi zaidi ya elfu moja (1,000) na baada ya awamu zote tatu kukamilika kiwanda kitaajili wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4,000).

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa amesema kuwa ofisi yake inashughulukia changamoto ya uvamizi wa ardhi kwa eneo walilopewa, na serikali ipo katika mpango wa kumuongezea eneo mwekezaji huyo mzawa kati ya hekta 12,000 zilizobakia baada ya kupewa hekta 10,000 ili kumaliza changamoto hiyo ya wavamizi wa ardhi.

...MWISHO...


Friday, 28 May 2021

UEFA FINAL GAME IN ENGLAND PITCH... CHELSEA vs MAN CITY

Ni masaa machache kushuhudia na kuikata kiu ya wanasoka wote Duniani kwa ujumla waliokaa kwa muda na wakingoja kujua ni nani atakuwa bigwa wa kumbe la Club Bingwa Barani Ulaya UEFA kati ya mahasimu wawili wa Ligi kuu Egland hapa inazungumziwa Chelsea na Manchester City

Thursday, 27 May 2021

Manchester United loss Europa agaist villarreal after 11 Penalt....

Moja kati ya tumaini kubwa lililokuwa likiwapa mashabiki wa Manchester United Duniani kote kiburi na jeuri ilikuwa kulichukua kombe maarufu duniani EUROPA LEAGUE.

Ila kama ilivyo ada kwamba siku huwa azigandi na ile misemo miwili maarufu kwenye mpira wa miguu zijulikanazo kama Mpira ni dakika Tisini Kweli zilianza kuanzia sekunde ya kwanza mpaka Dakika ya tisini ikiwa bado Mashabiki wa Manchester United wakiamini kwa timu waliyonayo basi bado wananafasi kubwa ya kupata ubingwa huo, ila kauli yapili ndiyo iliyowamaliza Manchester United (Mpira unadunda), Mambo yalikuwa magumu kwa timu zote mbili kupelekea dakika za nyongeza pia matokeo kuwa ni 1:1.

Haikuwa bahati kwa Manchester United kuingia kwenye Mikwaju ya penalt na hii ni baada ya Manchester kupoteza Mchezo huo na kulipoteza komba ambalo mashabiki wake duniani walikuwa wakilingoja, Nibaada ya Penalt 10 kuwa sawa kwenye Penalt ya 11 Villarreal wakaibuka washindi mara baada ya Golikipa wa Manchester United kukosa Penalt na Mwenzie wa Villarreal kushinda hivyo kupelekea Manchester kuwa nyuma ya Villarreal na kuwapa ruksa ya kutangazwa kuwa Mabingwa wapya wa kombe la Europa League

Thursday, 20 May 2021

DESKTOP SPECIFICATION FOR HOME AND OFFICE USE....

Hellow how are you there!, I hope you go through this post healthfully, Todays the world activity is converted to Computer based time to time, most of the work are done through the use of the computer thus the Computer become the Most Important device from personal level, office level, National level and Worldwide Level.

On this Post out Blogger try to explain Some if not all-Important factor to consider when buying a Desktop Computer for Home/Personal Use to office level.

MOTHERBOARD: Gigabyte B560M-DS3H Motherboard
POWER SUPPLY: Scaled appropriately to support delivered system with reasonable growth potential (In Win CE685 PC case with 300-watt 80PLUS certified power supply
CASE: In Win CE685 PC case with 300-watt 80PLUS certified power supply
CPU: Intel Core i5-11400 Processor
RAM: 8GB DDR4 2666 (PC4 21333) RAM (1 8GB DIMM) it is recommended the computer to have more than one RAM Slot.
NIC: On-board 10/100/1000 Mbps based Ethernet NIC
HDD: 250 GB Western Digital M.2 NVMe SSD Part # WDS250G2B0C
VIDEO: Integrated Intel HD Graphics with DVI Digital Output Interface
OPTICAL DRIVE: (optional)
AUDIO: Onboard HD audio (this is optional as not come with internal speaker but make sure the external speaker is working properly)
EXTERNALLY POWERED SATELLITE SPEAKERS: (optional)
6 EXTERNAL POWERED USB PORTS AND 2 ON FRONT OF CASE
OPERATING SYSTEM: Microsoft Windows 7 Home Basic (or other least expensive Microsoft Windows operating system) it can be above this OS not Limited to Maximum version only for Min-Version.
ALL APPROPRIATE CABLES NECESSARY HIDS: USB Optical mouse, mouse pad, USB keyboard, all necessary cables
WARRANTY 3-year parts and labor warranty on all components, and make sure the Condition for warranty is well explained on the manual book with your Device
MONITOR: 20″ Wide Screen LCD Monitor (1920×1080 native resolution) with DVI Digital Input Interface.

On the next Post we will describe the Factor for Personal Computer 🖥 (Laptop) For any Question, please Comment here down and our expert will come to chat with you direct to your email, also your allowed to ask for Specific Requirement of your Computer depend on what you want to do with it.

SIMBA FC DO or DIE SEASON 2

KAGERE; CHAMA; MIQUISO; BOKO; MORRISON TUMAINI LA SIMBA

Ikiwa ni siku mbili tuh simebaki kwa Simba kuipata hatima ya Timu yao kuendelea na michuano ya mabigwa afrika au kurudi kucheza mechi za ndani kama watani wao Yanga. Japo ni ngumu ila wachezaji wa Simba pamoja na Kocha wao Gomez wamesema haya katika mahojiono na waandishi tofauti tofauti wa habari "Nikweli tuna mlima mkubwa wa kupanda ili kuendelea na safari yetu ya michuano hii ya mabigwa wa soka barani Afrika lakini hatujalala wala kukata tamaa tangu tumerejea kutoka Afrika ya Kusini na tupo kwenye mazoezi ya kufa na kupona kuhakikisha tunapanda kilima hicho cha ushindi wa goli 5 kwa o katika uwanja wetu wa nyumbani Pale kwa Mkapa! na kurudisha imani ya mashabiki wetu ikiwa ni sambamba na kupata tiketi ya kuendelea katika hatua ya nusu fainali"

Hiyo ndio kauli ya Simba kwa ujumla kwa sasa ikiwa ni njia ya kutiana moyo na kuongeza maandalizi katika kuwania nafasi ya kuingia katika hatua ya nusu fainali na hatimaye fainali ya Kombe la mabingwa afrika.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Simba FC

Monday, 17 May 2021

DIMBA LA KWAMKAPA TUMAINI PEKEE LA SIMBA NUSU FAINALI....

Ikiwa ni mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabigwa barani Africa ambapo Simba FC iliyokuwa tegemezi kwa taifa la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwani ndiyo ilikuwa ikituwakilisha kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na ilikuwa imefanya vizuri kabisa katika Michuano hii mwaka huu wa 2020/2021.

Simba FC Juzi tarehe 15.05.21 ilijikuta ikikutana na kipigo cha goli nne bila kupata goli hata moja lakufutia machozi vijana hao wa Simba walipokea kipigo hicho ikiwa ni mzunguko wa kwanza wa Robo Fainali na mechiu hiyo ilikuwa ugenini na siku si nyingi watakuja kwa Mkapa Dar es Salaam na humo dimbani ndio dakika tisini au 120 au Penalt zitasema nani aendelee mbele nani asubiri msimu ujao kati ya wana sport hao wa timu ya Afrika Kusini (Kaizer Chief FC) na Simba Fc ya Tanzania mwenyeji wa mchezo huo.

Simba kupitia msemaji wake mkuu Haji Manara amesema Simba kupoteza mchezo ule ni sawa mwanachuyo kufeli mtihani na bado akawa ananafasi moja mezani ya kuurudia mtihani ule, Haya aliyasema akijibu kejeli za watani wao wa Yanga FC waliopata matokeo ya Suluhu wakiwa kanda ya Kusini mwa nchi ya Tanzania, nawao hawakuangalia matokeo yao Aliyoyaita msemaji wa Simba kwamba ni sawa na kufeli darasa la saba, mbali na hapo kuitupia maneno tuh timu ya Simba FC moja kwa moja.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba, Kwamkapa ikawe njia ya Nusu Fainali...

Wednesday, 12 May 2021

SAKATA LA CHANJO YA CORONA BUNGENI...

Mara baada ya Raisi wa awamu ya sita Mh. Samia Suluhu Hassan kuapishwa na kuwa raisi wa nchi ya Tanzania alitangaza kuunda kamati maalum ya kuchunguza maradhi mapya ya Corona unajulikana kama Covid 19 ulioibuka December 2019 nchini China na baadae kusambaa takribani duniani kote.


Nchi ya Tanzania ikiwa chini ya uongozi wa Dr. Magufuli, aliamua kutangaza kutokukubaliana  kwa namna yeyote dhidi maradhi ya Corona na kubwa zaidi Tanzania ikawa tofauti na nchi nyingi duniani baada ya kutangaza kwamba hakutakuwa na Lockdown yoyote na akiamuru ratiba zote zirudi kama awali kabla ya kuibuka Corona na hapo mipaka yote ikawekwa wazi na ofisi zote kufunguliwa bila kusahau shule na vyuo vyote kufunguliwa na mambo yakawa sawa kabisaa. Na wanasema Mungu si Athumani basi kila kukicha Tanzania ikawa ikishuka idadi ya wagonjwa wa Corona na kufikia 0% ya taarifa ya vifo na waathirika wa janga la Corona... Amiin Mwenyezi Mungu alitusimamia na anazidi kutukingia mkono, tuzidi kumtumainia yeye na kuamini kwamba yeye ni muweza wa yote.


Ila baada ya kamati kuundwa na kuja na taarifa bungeni ni wazi kwamba inashauri kuikubali Corona na kuanza kuchukua hatua dhidi ya janga hilo ikiwemo na kutafakari chanjo ya kuwapatia watanzania. Je hii kwako imekaaje?


Baadhi ya wabunge wa bunge tukufu la Tanzania wamelisemea hili bungeni na moja ya mmbunge aliyepata nafasi na kuzungumza vyakutosha ni mmbunge wa Kawe jijini Dar es salaam na kujaribu kuzielezea baadhi ya chanjo ambazo huenda mojawapo ikachaguliwa kutumika nchini kwetu. Nanukuu "Ukweli ni kwamba chanjo zote zinazotumika duniani zimepitishwa na mashirika ya dawa ya dharura mbali na hilo zote bado zinatumika huku zikiwa kwenye majaribio" Amewaomba wataalamu wa nchi kuzichunguza zaidi ikifungamana na kutazama madhara tunayopitia sasa yakutokuwa na chanjo na yale tutakayoyapata kutokamana na chanjo hizo! Hivyo basi kujaribu kuwa wavumilivu na kutizama madhara ya miaka kadhaa ijayo kwa wale watakaokuwa wametumia chanjo hizo. Hii hapa video ya Mh. Gwajima akiwa bungini watch out!

Ni muda sahihi watanzania kuungana na kushauri kuhusu maradhi haya ikiwa ni pamoja na kumtanguliza Mungu wetu tunayeamini anaweza na yupo juu ya kila jambo.


40's YEAR's OF BOB MARLEY IN HEAVEN...

Bob Marley ni mzawa wa Jamaica aliyejulikana duniani kote kama mfalme wa muziki wa Reggae ambapomkapa sasa bado Miziki yake inasikika katika sehemu mbali mbali licha ya kuondoka kwake miaka 40 iliyopita.

Bob alizaliwa 06/02/1945 na alifariki tarehe kama ya leo 11/05/1981, Ikiwa ni miaka 40 tangu kifo chake ila bado Muziki wake unaendele kusikilizwa katika kizazi cha leo! mpaka sasa bado kuna sababu ya wasanii kutafuta njia za kuimba muziki kama alivyokuwa akifanya ngulii Bob Marley.

Zipo sababu nyingi zinazopelekea Muziki wa Bob Marley kuendelea kuwa Licha ya yeye mwenyewe kuwa amepoteza maisha miaka 40 iliyopita kubwa ni ujumbe Miziki aliyoimba Bob Marley imekuwa wakati wote ikibeba jumbe mbali mbali ambazo zimekuwa ni fundisho sana kwenye jamii na alikuwa akiimba kutokana na matukio halisi ya kwenye jamii, Pia mbali na ujumbe uliopo ndani ya Muziki wa Bob alikuwa akitumia mistari / Mashairi isiyo na Lugha Chafu, Hii imekuwa ikifanya mziki wake kusikilizwa na watu wa rika zote na Jinsia zote.

Hakika hatuta msahau Bob Marley katika Niyimbo zake zilizokuwa zikibeba ujumbe wa aina yeke haswa ilikuwa ni Kuwasihi watu wa Africa kuungana na kutafuta uhuru wao, pamoja na yele mashairi aliyokuwa akiandika na kumsifu mwanamke pamoja na kutaja sifa zake kuieleza jamii Mwanamke ni nani na anapaswa kupewa thamani gani.

Pia alijitahidi kuhusia upendo na amani kwa wanadamu wote kuacha ubaguzi wa dini, jinsi, rangi, utaifa, na ukabila akisisitiza kwamba sisi wote ni sawa na tunakila sababu ya kupendana na kuheshimiana.

R.I.P BOB MARLEY

SIMBA FC YATUA KIBABE SOUTH AFRICA...

Hii ni baada ya tarehe kuwa zimekaribia (15.05.2021) kwa Timu nane bingwa Afrika kuchuana katika kutimiza hatua ya Robo Fainali ya Club Bingwa Africa, Simba Sport Club, kama ilivyo ada teari wameshawasili South Africa kwaajili ya kuvaana na wataalamu wa soka nchini humo Kaizer Chiefs.

Simba kibabe kabisa jana waliondoka nchini jumla ya wachezaji 24 pamoja na benchi la ufundi bila kuwa mbali na msemaji mkuu wa timu hiyo gwiji wa mpira kwa sasa nchini Tanzania Bw.Haji Manara. Uongozi wa Simba FC umeviambia vyombo vya habari mbali mbali kwamba kuna mambo kadha wa kadha dhidi ya nyota wa soka la mpira wa miguu Benard Morrison ambayo yanaendelea kuwekwa sawa na muda wowote ataanza safari kuelekea south africa ili kuhakikisha wanakuwa na mwanzo mzuri wa hatua hii ya Robo fainali Club Bingwa Arica.

Mungu Ibariki Simba, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa Mashariki!

Tuesday, 11 May 2021

FAIDA ZA KUCHEZA GAME'S KWA WATOTO NA WATU WAZIMA...

Je! wajua yakwamba kutokana na kuongezeka vifaa vya kumpyuta vimepelekea Games kuwa ni sehemu ya maisha kwa watu wa rika zote kuanzia watoto vijana na hata watuwazima pia haibagua kwenye suala la jinsia wanaume kwa wanawake wote hucheza games. Hii imetokana na kuwapo kwa Faida nyingi kwa wachezaji.

Uwepo wa Games umeleta maswali mengi haswa kwa wazazi na walezi wa watoto na wengi wao kubaki njia panda bila kujua kwamba kuna faida ya kucheza Games au ni hasara tupu, na je kama faida zipo ni zipi wengi wamekuwa wakitaka kujua. kupitia Blogu yako pendwa kabisa leo tutakuanishia Faida chache tuh ikiwa ni mwanzo wakufanya watu kufikiria mchezo wa Game katika mawazo chanya.

Zipo faida nyingi sana zakucheza games kwa Mtu mzima na haswa kwa watoto wetu haswa na leo ntaanza kwa kukupatia faida kuu tano anazopata Mtu pale achezapo games na hii imezingatia zaidi kwenye Games za kwenye Kompyuta na vifaa vya aina yake.

(1)KUBORESHA UJUZI WA KUJIFUNZA. Michezo ya games haswa kwenye game za kisasa zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kabisa na hivyo huhitaji matumizi makubwa ya fikra na uwezo wakijifunza jambo jipya ili kuweza kucheza aina tofauti tofauti za games zinazotoka kila siku, hivyo haswa kwa mtoto au mwanafunzi anayecheza games anakuwa na uwezomkubwa wa kujifunza ujuzi mpya kulinganisha na yule ambaye si mchezaji.

(2)HUONGEZA UWEZO WA KUTATUA CHANGAMOTO. Kama wewe nimfuatiliaji wa game nyingi za kisasa (Modern games) utagundua ya kwamba imejaa ndaniyake changamoto nyingi na kumtaka mchezaj wa game hiyo kupambana na kuzitatua changamoto ili kuendelea kucheza na kujiongezea alama za ushindi, hivyo basi hii humuongezea mchezaji uwezo wakupambana na matatizo mengine yanayomkuta kwenye maisha halisi

(3)HUONGEZA AFYA YA AKILI Wataalamu waliofanya utafiti kati ya wecheza Games na wale wasiojihusisha na michezo hiyo ni kwamba mwenye kucheza game anakuwa na Afya zaidi ya akili na hii hutokana na kwamba muda wote anapokuwa kwenye mchezo wa Games basi akili huwa inatulia na kubaki kwenye Kiyoo cha game tu!

(4)HUPUNGUZA / KUMALIZA TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO Moja kati ya tatizo lilalowakumba watu wengi Dunia ya leo ni msongo wa mawazo, na hii hutokea bila hata watu wengine kujua na inamazara makubwa. lakini kwa kuwa mtu mwenye taratibu za kucheza game basi kitaalamu huondoa msongo wamawazo kwa mchezaji na kukuweka fresh kiakili kufanya mambo mengine

(5)HUMJENGEA MCHEZAJI KUJIAMINI Game ni moja ya mchezo unaomruhusu mchezaji kufanya kile anachohisi ni sahihi kwani anakuwa maranyingi yupo pekeyake au laa anakuwa yupo na mtu aliyenauhuru naye hivyo kutokuwa na woga wakujaribu na hii humfanya kuona anaweza na mawazoyake ni sahihi hivyo basi humjengea kujiamini hata kwenye maisha yakila siku. (Mfano kucheza game na mwanao inamfanya sio kukupa challenge kwenye game tu ila hata nje ya game anakuwa anaweza kuchania mawazo mbele yako kama mzazi.)

PAMOJA NA FAIDA ZA GAME PIA ZIPO HASARA ZA MTU KUCHEZA GAME! Hasara kubwa ya Game ni pale mtu haswa mtoto anapokwa Mraibu wa Games Hii hupelekea kupoteza muda na kupitwa na mambo ya msingi kama vile kutokupitia masomoyake muda wa jioni, na kubwa zaidi ni mtoto kuchelewa sana kulala na hivyo kumfanya Siku inayofuata kushinda na uchovu na kushindwa kutimiza majukumu yake ya msingi.

MTOTO ALIYECHEZA GAME HADI KULALA KWENYE MEZA!

Monday, 10 May 2021

BAGAMOYO SUGAR FC...

Picha ya pamoja ya wachezaji wa Team ya Bagamoyo Sugar FC baada ya Bonanza la uzinduzi wa Jezi.

Bagamoyo Sugar Ltd, kampuni iliyopo mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo - Makurunge inayomilikiwa na Azam Bakhresa Group of Companies.

Kampuni hiyo ikiwa bado haijaanza kutoa bidhaa ya Sukari lakini mambo ynazidi kupamba moto na Mwezi wasita mwakani inatarajiwa kuanza kutoa Bidhaa ya Sukari na hii itapunguza au kumaliza kiasi cha sukari kinachoagizwa kutoka nchi za nje.

Jana Mnamo majira ya saakumi jioni kulikuwa na uzinduzi wa jezi za kwanza kakbisa za timu hiyo zilizozaminiwa na Bakhresa group of Companies (AZAM), Katika uzinduzi kulikuwa na mechi kati ya Timu mbiliManagement na Supervisor's VS Madeva na Maoperator's Mchezo uliochezwa katika viwanja vya bagamoyo mijini majira ya Saakumi jioni, na Hatimaye Timu ya Management and Supervisor ikaibuka kidedea kwa Ushindi wa bao mbili kwa moja (2-1).

Golilakwanza likifungwa kwa njia ya mpira wa adhabu baada ya kufanyiwa Rafu Afisa Rasilimali Watu Mr. Abdi na baadaye kipindi cha pili Foward wa timu hiyo ya Managemenet and Supervisor Ikajipatia goli lake la ushindi kutoka kwa Mshambuliaji wake Ibrahimu

Pichani ni baadhi ya wachezaji wa timu Management and Supervisor's katika kupanga mbinu za mapambano baada ya kipindi cha kwanza kutoa suluhu ya moja moja.

SEREKALI YATOA TAMKO LEO KUHUSU KUAGHIRISHWA MECHI YA WATANI WA JADI...

Bungeni leo tarehe 10 mwezi wa 5 mwaka 2021 Serekeli kupitia kwa wazirimkuu (ambaye ni shabiki kindaki ndaki wa mpira wa miguu na ni mpenzi na mzalendo wa wazi wazi kwenye ligi kuu ya nchi Tanzania Vodacom Premier Legue.

Amemtaka waziri wa habari na michezo kuweza kutoa tamko ikiwamo ni pamoja na kuweka wazi sababu ya kubadilika kwa muda na hatimaye kuaghirishwa kwa mechi ya watani wa jadi Kariakoo Derby ikiwa na sambamba na kuutangazia umaa ni hatua zipi zimechukuliwa na mechi itakuwa lini.

Taarifa hii inawataka mashabiki wote wa mpira duniani kuwa wavumilivu na kutambua Serekali inatambua kwamba kuja jambo lililotendeka ambalo sio sawa na linafanyiwa kazi na mwisho ufafanuzi utatolewa kupitia Wizira husika.

TFF WAOMBA RADHI KUAGHIRISHWA KWA MECHI NA KUIGEUKIA BODI YA LIGI KUU TANZANIA...

Mnamo tarehe 8 mwezi wa tano siku ya jumamosi Watanzania na watu kutoka nchi za jirani walifika katika viwanja vya kwamkapa jijini Dar es salaam kwaajili ya kushuhudia mechi ya watani wajadi maarufu kama Kariakoo Derby. Inayowakutanisha mahasimu wawili wa mpira wamiguu Tanzania hapa naizungumzia simba na Yanga.

Mechi ilikuwa ichezwe majira ya saakumi na moja ya jioni ila hatimaye dakika chache kabla ya muda wa mechi kufika palitokea sintofahamu baada ya Tangazo kutoka kwamba mechi haitachezwa katika muda uliokuwa umetangazwa na badala yake itachezwa mida ya saamoja kamili usiku katika uwanja huo huo.

Mara baada ya taatifa hiyo pakazuka taharuki ambapo mpaka leo bado mambo hayajakaa sawa ni baada ya timu ya Yanga kubaki uwanjani kwa dakika kadhaa baada ya muda wa awali na majira ya takribani saa 11:30 jioni Wachezaji wa yanga walitimka na kuondoka uwanjani ishara ya kuisusa mechi na muda huo huo wahasimu wao Simba FC wakaingia uwanjani tayari kuanza kupasha misuli kwaajili ya mechi saamoja kamili.

Nimudamchache baadae ikasemekana yanga kutangaza kutokucheza meche hiyo kwa kile kilichodaiwa kuishinikiza TFF wamevunja sheria mara baada ya kubadili muda wa mechi hiyo dakika chache kabla ya mechi kuanza wakati sheria inasema ratiba ya mechi itabadilishwa masaa 24 kabla ya muda wa mechi kufika.

Kutokana na halihiyo mengi yamesemwa ila TFF nao hawajabaki nyuma kwautangulizi Uongozi wa TFF wameomba radhi kwa Mashabiki wote hususan wa mpira wa miguu waliokuwa wamejiandaa kuangalia au kusikiliza mechi hiyo yenye mashabiki wengi kuliko Tanzania na Afrika Mashariki kwa usumbufu uliyojitokeza, hawakuishia hapo uongozi huo wa TFF pia umeitaka Bodi ya ligi kuu Tanzania bara kutoa tamko kuhusu sababu zilizopilekea mchezo huo kutochezwa siku na muda husika na hatimaye kuaghirishwa na kutojulikana utachezwa lini.

Saturday, 8 May 2021

DABI SIMBA NA YANGA KWA MKAPA LEO 8.5.21

Nikwamara ya pili wanakutana Wahasimu wa mpira wa miguu katika uwanja wa kwa Mkapa katika mechi za mzunguko wa pili wa likikuu Tanzania bara. 

Nisiku chache mara baada ya Simba kukaa kileleni mwa ligi baada ya kupishwa na wahasimu wao hao wa mpira wa miguu Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania na Amani ipatikane katika mchezo huu wa watani wetu wa jadi!

mwanganews bloggers we are online to update our visitors!