Mechi ilikuwa ichezwe majira ya saakumi na moja ya jioni ila hatimaye dakika chache kabla ya muda wa mechi kufika palitokea sintofahamu baada ya Tangazo kutoka kwamba mechi haitachezwa katika muda uliokuwa umetangazwa na badala yake itachezwa mida ya saamoja kamili usiku katika uwanja huo huo.
Mara baada ya taatifa hiyo pakazuka taharuki ambapo mpaka leo bado mambo hayajakaa sawa ni baada ya timu ya Yanga kubaki uwanjani kwa dakika kadhaa baada ya muda wa awali na majira ya takribani saa 11:30 jioni Wachezaji wa yanga walitimka na kuondoka uwanjani ishara ya kuisusa mechi na muda huo huo wahasimu wao Simba FC wakaingia uwanjani tayari kuanza kupasha misuli kwaajili ya mechi saamoja kamili.
Nimudamchache baadae ikasemekana yanga kutangaza kutokucheza meche hiyo kwa kile kilichodaiwa kuishinikiza TFF wamevunja sheria mara baada ya kubadili muda wa mechi hiyo dakika chache kabla ya mechi kuanza wakati sheria inasema ratiba ya mechi itabadilishwa masaa 24 kabla ya muda wa mechi kufika.
Kutokana na halihiyo mengi yamesemwa ila TFF nao hawajabaki nyuma kwautangulizi Uongozi wa TFF wameomba radhi kwa Mashabiki wote hususan wa mpira wa miguu waliokuwa wamejiandaa kuangalia au kusikiliza mechi hiyo yenye mashabiki wengi kuliko Tanzania na Afrika Mashariki kwa usumbufu uliyojitokeza, hawakuishia hapo uongozi huo wa TFF pia umeitaka Bodi ya ligi kuu Tanzania bara kutoa tamko kuhusu sababu zilizopilekea mchezo huo kutochezwa siku na muda husika na hatimaye kuaghirishwa na kutojulikana utachezwa lini.
No comments:
Post a Comment