Wednesday, 12 May 2021
SIMBA FC YATUA KIBABE SOUTH AFRICA...
Hii ni baada ya tarehe kuwa zimekaribia (15.05.2021) kwa Timu nane bingwa Afrika kuchuana
katika kutimiza hatua ya Robo Fainali ya Club Bingwa Africa,
Simba Sport Club, kama ilivyo ada teari wameshawasili South Africa
kwaajili ya kuvaana na wataalamu wa soka nchini humo Kaizer Chiefs.
Simba kibabe kabisa jana waliondoka nchini jumla ya wachezaji 24 pamoja na
benchi la ufundi bila kuwa mbali na msemaji mkuu wa timu hiyo gwiji wa mpira kwa
sasa nchini Tanzania Bw.Haji Manara. Uongozi wa
Simba FC umeviambia vyombo vya habari mbali mbali kwamba kuna mambo kadha
wa kadha dhidi ya nyota wa soka la mpira wa miguu Benard Morrison ambayo
yanaendelea kuwekwa sawa na muda wowote ataanza safari kuelekea south africa ili
kuhakikisha wanakuwa na mwanzo mzuri wa hatua hii ya Robo fainali Club Bingwa
Arica.
Labels:
Sports
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment