Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba, Kwamkapa ikawe njia ya Nusu Fainali...
Monday, 17 May 2021
DIMBA LA KWAMKAPA TUMAINI PEKEE LA SIMBA NUSU FAINALI....
Ikiwa ni mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabigwa barani Africa ambapo Simba FC iliyokuwa tegemezi kwa taifa la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwani ndiyo ilikuwa ikituwakilisha kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na ilikuwa imefanya vizuri kabisa katika Michuano hii mwaka huu wa 2020/2021.
Simba FC Juzi tarehe 15.05.21 ilijikuta ikikutana na kipigo cha goli nne bila kupata goli hata moja lakufutia machozi vijana hao wa Simba walipokea kipigo hicho ikiwa ni mzunguko wa kwanza wa Robo Fainali na mechiu hiyo ilikuwa ugenini na siku si nyingi watakuja kwa Mkapa Dar es Salaam na humo dimbani ndio dakika tisini au 120 au Penalt zitasema nani aendelee mbele nani asubiri msimu ujao kati ya wana sport hao wa timu ya Afrika Kusini (Kaizer Chief FC) na Simba Fc ya Tanzania mwenyeji wa mchezo huo.
Simba kupitia msemaji wake mkuu Haji Manara amesema Simba kupoteza mchezo ule ni sawa mwanachuyo kufeli mtihani na bado akawa ananafasi moja mezani ya kuurudia mtihani ule, Haya aliyasema akijibu kejeli za watani wao wa Yanga FC waliopata matokeo ya Suluhu wakiwa kanda ya Kusini mwa nchi ya Tanzania, nawao hawakuangalia matokeo yao Aliyoyaita msemaji wa Simba kwamba ni sawa na kufeli darasa la saba, mbali na hapo kuitupia maneno tuh timu ya Simba FC moja kwa moja.
Labels:
Sports
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment