Tuesday, 11 May 2021

FAIDA ZA KUCHEZA GAME'S KWA WATOTO NA WATU WAZIMA...

Je! wajua yakwamba kutokana na kuongezeka vifaa vya kumpyuta vimepelekea Games kuwa ni sehemu ya maisha kwa watu wa rika zote kuanzia watoto vijana na hata watuwazima pia haibagua kwenye suala la jinsia wanaume kwa wanawake wote hucheza games. Hii imetokana na kuwapo kwa Faida nyingi kwa wachezaji.

Uwepo wa Games umeleta maswali mengi haswa kwa wazazi na walezi wa watoto na wengi wao kubaki njia panda bila kujua kwamba kuna faida ya kucheza Games au ni hasara tupu, na je kama faida zipo ni zipi wengi wamekuwa wakitaka kujua. kupitia Blogu yako pendwa kabisa leo tutakuanishia Faida chache tuh ikiwa ni mwanzo wakufanya watu kufikiria mchezo wa Game katika mawazo chanya.

Zipo faida nyingi sana zakucheza games kwa Mtu mzima na haswa kwa watoto wetu haswa na leo ntaanza kwa kukupatia faida kuu tano anazopata Mtu pale achezapo games na hii imezingatia zaidi kwenye Games za kwenye Kompyuta na vifaa vya aina yake.

(1)KUBORESHA UJUZI WA KUJIFUNZA. Michezo ya games haswa kwenye game za kisasa zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kabisa na hivyo huhitaji matumizi makubwa ya fikra na uwezo wakijifunza jambo jipya ili kuweza kucheza aina tofauti tofauti za games zinazotoka kila siku, hivyo haswa kwa mtoto au mwanafunzi anayecheza games anakuwa na uwezomkubwa wa kujifunza ujuzi mpya kulinganisha na yule ambaye si mchezaji.

(2)HUONGEZA UWEZO WA KUTATUA CHANGAMOTO. Kama wewe nimfuatiliaji wa game nyingi za kisasa (Modern games) utagundua ya kwamba imejaa ndaniyake changamoto nyingi na kumtaka mchezaj wa game hiyo kupambana na kuzitatua changamoto ili kuendelea kucheza na kujiongezea alama za ushindi, hivyo basi hii humuongezea mchezaji uwezo wakupambana na matatizo mengine yanayomkuta kwenye maisha halisi

(3)HUONGEZA AFYA YA AKILI Wataalamu waliofanya utafiti kati ya wecheza Games na wale wasiojihusisha na michezo hiyo ni kwamba mwenye kucheza game anakuwa na Afya zaidi ya akili na hii hutokana na kwamba muda wote anapokuwa kwenye mchezo wa Games basi akili huwa inatulia na kubaki kwenye Kiyoo cha game tu!

(4)HUPUNGUZA / KUMALIZA TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO Moja kati ya tatizo lilalowakumba watu wengi Dunia ya leo ni msongo wa mawazo, na hii hutokea bila hata watu wengine kujua na inamazara makubwa. lakini kwa kuwa mtu mwenye taratibu za kucheza game basi kitaalamu huondoa msongo wamawazo kwa mchezaji na kukuweka fresh kiakili kufanya mambo mengine

(5)HUMJENGEA MCHEZAJI KUJIAMINI Game ni moja ya mchezo unaomruhusu mchezaji kufanya kile anachohisi ni sahihi kwani anakuwa maranyingi yupo pekeyake au laa anakuwa yupo na mtu aliyenauhuru naye hivyo kutokuwa na woga wakujaribu na hii humfanya kuona anaweza na mawazoyake ni sahihi hivyo basi humjengea kujiamini hata kwenye maisha yakila siku. (Mfano kucheza game na mwanao inamfanya sio kukupa challenge kwenye game tu ila hata nje ya game anakuwa anaweza kuchania mawazo mbele yako kama mzazi.)

PAMOJA NA FAIDA ZA GAME PIA ZIPO HASARA ZA MTU KUCHEZA GAME! Hasara kubwa ya Game ni pale mtu haswa mtoto anapokwa Mraibu wa Games Hii hupelekea kupoteza muda na kupitwa na mambo ya msingi kama vile kutokupitia masomoyake muda wa jioni, na kubwa zaidi ni mtoto kuchelewa sana kulala na hivyo kumfanya Siku inayofuata kushinda na uchovu na kushindwa kutimiza majukumu yake ya msingi.

MTOTO ALIYECHEZA GAME HADI KULALA KWENYE MEZA!

No comments:

Post a Comment