Wednesday, 12 May 2021

SAKATA LA CHANJO YA CORONA BUNGENI...

Mara baada ya Raisi wa awamu ya sita Mh. Samia Suluhu Hassan kuapishwa na kuwa raisi wa nchi ya Tanzania alitangaza kuunda kamati maalum ya kuchunguza maradhi mapya ya Corona unajulikana kama Covid 19 ulioibuka December 2019 nchini China na baadae kusambaa takribani duniani kote.


Nchi ya Tanzania ikiwa chini ya uongozi wa Dr. Magufuli, aliamua kutangaza kutokukubaliana  kwa namna yeyote dhidi maradhi ya Corona na kubwa zaidi Tanzania ikawa tofauti na nchi nyingi duniani baada ya kutangaza kwamba hakutakuwa na Lockdown yoyote na akiamuru ratiba zote zirudi kama awali kabla ya kuibuka Corona na hapo mipaka yote ikawekwa wazi na ofisi zote kufunguliwa bila kusahau shule na vyuo vyote kufunguliwa na mambo yakawa sawa kabisaa. Na wanasema Mungu si Athumani basi kila kukicha Tanzania ikawa ikishuka idadi ya wagonjwa wa Corona na kufikia 0% ya taarifa ya vifo na waathirika wa janga la Corona... Amiin Mwenyezi Mungu alitusimamia na anazidi kutukingia mkono, tuzidi kumtumainia yeye na kuamini kwamba yeye ni muweza wa yote.


Ila baada ya kamati kuundwa na kuja na taarifa bungeni ni wazi kwamba inashauri kuikubali Corona na kuanza kuchukua hatua dhidi ya janga hilo ikiwemo na kutafakari chanjo ya kuwapatia watanzania. Je hii kwako imekaaje?


Baadhi ya wabunge wa bunge tukufu la Tanzania wamelisemea hili bungeni na moja ya mmbunge aliyepata nafasi na kuzungumza vyakutosha ni mmbunge wa Kawe jijini Dar es salaam na kujaribu kuzielezea baadhi ya chanjo ambazo huenda mojawapo ikachaguliwa kutumika nchini kwetu. Nanukuu "Ukweli ni kwamba chanjo zote zinazotumika duniani zimepitishwa na mashirika ya dawa ya dharura mbali na hilo zote bado zinatumika huku zikiwa kwenye majaribio" Amewaomba wataalamu wa nchi kuzichunguza zaidi ikifungamana na kutazama madhara tunayopitia sasa yakutokuwa na chanjo na yale tutakayoyapata kutokamana na chanjo hizo! Hivyo basi kujaribu kuwa wavumilivu na kutizama madhara ya miaka kadhaa ijayo kwa wale watakaokuwa wametumia chanjo hizo. Hii hapa video ya Mh. Gwajima akiwa bungini watch out!

Ni muda sahihi watanzania kuungana na kushauri kuhusu maradhi haya ikiwa ni pamoja na kumtanguliza Mungu wetu tunayeamini anaweza na yupo juu ya kila jambo.


No comments:

Post a Comment