R.I.P BOB MARLEY
Wednesday, 12 May 2021
40's YEAR's OF BOB MARLEY IN HEAVEN...
Bob Marley ni mzawa wa Jamaica aliyejulikana duniani kote kama mfalme wa muziki wa Reggae ambapomkapa sasa bado Miziki yake inasikika katika sehemu mbali mbali licha ya kuondoka kwake miaka 40 iliyopita.
Bob alizaliwa 06/02/1945 na alifariki tarehe kama ya leo 11/05/1981, Ikiwa ni miaka 40 tangu kifo chake ila bado Muziki wake unaendele kusikilizwa katika kizazi cha leo! mpaka sasa bado kuna sababu ya wasanii kutafuta njia za kuimba muziki kama alivyokuwa akifanya ngulii Bob Marley.
Zipo sababu nyingi zinazopelekea Muziki wa Bob Marley kuendelea kuwa Licha ya yeye mwenyewe kuwa amepoteza maisha miaka 40 iliyopita kubwa ni ujumbe Miziki aliyoimba Bob Marley imekuwa wakati wote ikibeba jumbe mbali mbali ambazo zimekuwa ni fundisho sana kwenye jamii na alikuwa akiimba kutokana na matukio halisi ya kwenye jamii, Pia mbali na ujumbe uliopo ndani ya Muziki wa Bob alikuwa akitumia mistari / Mashairi isiyo na Lugha Chafu, Hii imekuwa ikifanya mziki wake kusikilizwa na watu wa rika zote na Jinsia zote.
Hakika hatuta msahau Bob Marley katika Niyimbo zake zilizokuwa zikibeba ujumbe wa aina yeke haswa ilikuwa ni Kuwasihi watu wa Africa kuungana na kutafuta uhuru wao, pamoja na yele mashairi aliyokuwa akiandika na kumsifu mwanamke pamoja na kutaja sifa zake kuieleza jamii Mwanamke ni nani na anapaswa kupewa thamani gani.
Pia alijitahidi kuhusia upendo na amani kwa wanadamu wote kuacha ubaguzi wa dini, jinsi, rangi, utaifa, na ukabila akisisitiza kwamba sisi wote ni sawa na tunakila sababu ya kupendana na kuheshimiana.
Labels:
Celebrities
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment